RAGE AFUNGUA TAWI SIMBVA TISHIO KIBAHA.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/25-Feb-13/18:50:15 Mwenyekiti wa klabu ya Simba maarufu kama wekundu wa Msimbazi amezindua rasmi tawi namba 11 la SIMBA TISHIO lillilopo Katika Mtaa wa Kwa mfipa mjini Kibaha na kuongea na wanachama na washabiki wa timu hiyo mjini Kibaha. Akizungumza katika mkutano huo amewataka wana simba kutoachia klabu hiyo watu wasio na uwezo wa kifedha kutokana na mpira kwa hivi sasa kutawaliwa na fedha, amebainisha uwepo wa gharama mbalimbali ambazo wakati mwingine inakuwa haina uwezo wa kifedha kuzilipa na kama kiongozi unahitajika wakati wote kuwa na jibu muafaka kuhusiana na kila kinachotokea klabuni. Mwenyekiti RAGE amesikitishwa na baadhi ya magazeti ya Michezo kwa kupotosha taarifa mbalimbali kwa lengo la kutaka kuuza magazeti na kuwachanganya wapenzi na washabiki wa soka, akitoa mfano habaria ambayo gazeti moja la michezo nchini lilitoa ya kuwa Malkia wa Nyuki hawahitaji RAGE na KABURU kitu ambacho sio kweli Kabisa. Naye Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM ambaye pia ni shabiki mkubwa wa Wekundu wa Msimbazi BW. RUGEMALIRA RUTATINA amewataka uongozi wa Simba kufanya utaratibu wa kutembea na wachezaji wanapokuwa katikja safari kama aliyofanya Mjini Kibaha ili wapenzi na washabiki wao waweze kubadilishana nao mawazo na hata kupata nafasi za kukutana na kamati za ufundi za matawi. END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA