M4C NA POLICE WAAGANA
Ben Komba/Pwani-Tanzania/10-Feb-13/13:42:54
Chama cha demokrasia na maendeleo kimewataka wananchi kutokubali kurubuniwa kwa kuwaambia CHADEMA ni chama cha kidini kunakosababishwa kwa baadhi ya vyama kutumia propaganda hiyo kutaka kuwagawa watanzania na baadaye kuwatawala kwa kufuata mifumo ya kurithishana kama inavyojidhihirisha hivi sasa.
Akiongea katika mkutano wa vuguvugu la mabadiliko inayoendelea nchi hivi sasakatika viwanja vya stendi ya Mzenga katika mamlaka ya mji mdogo wa Mlandizi yenye kulenga kutekeleza kauli ya mwaka wa nguvu ya umma inayoeendeshwa na chama cha demokrasia na kufanikiwa kuleta mitazamo chanya kwa wakazi wa wilaya ya Kibaha kutokana na kuwepo piga nikupige ya mikutano kati ya chama cha CHADEMA na CCM.
Kada wa chama cha demokrasia na maendeleo kutoka Arusha, BW.ALLY BANANGA amesema cha cha CCM kimekuwa chama cha kurithisha uongozi na kuyatupa kando malengo ya awali ya uanzishaji wa chama hicho ambayo yalikuwa hayana lengo la kujenga himaya za kisultani kwa baadhi ya viongozi na familia zao kama ilivyo hivi sasa kwa kuzusha mambo ambayo hayana ukweli wowote katika kujaribu kuwagawa watanzania kiimani.
BW. BANANGA amebainisha kumekuwepo na harakati kubwa katika kuhakikisha wanafanikiwa kukamata dola mwaka 2015 na kuwaasa wana Kibaha ambo wamechoka kunyanyaswa na kukandamizwa na chama tawala kuunga mkono harakati hizo za CHADEMA zenye lengo la kumkomboa mtanzania na mgogoro mkubwa wa kimfumo tunaokabiliana nao kutokana na baadhi ya watu kujiona kama wana hati miliki na Taifa hili.
------------------------------------------------------END ------------------------------------
Ben Komba/Pwani-Tanzania/10-Feb-13/08:56:59
Jeshi la Polisi katika Mkoa wa Pwani limetakiwa kuendeleza ushirikiano miongoni mwaao ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila katika suala zima la kulinda utulivu na amani iliyopo.
Kamanda wa Polisi Kamishna msaidizi ERNEST MANGU ameyasema wakati wa hafla ya kumuaga baada ya kuhamishiwa katika Jiji la Mwanza, amesema kwa kufanya kazi kwa kushirikiana na upendo kutawezesha Jeshi hilo kuendelea kupata mafanikio.
Kamishna msaidizi MANGU ameongeza kwa kuwataka askari katika mkoa wa Pwani kutoa ushirikiano kwa kamanda mpya wa Jeshi hilo katika Mkoa wa Pwani, Kamishna msaidizi URLICH MATEI katika kuendeleza jukumu la kuwalinda wananchi na mali zao.
Awali akizungumza katika hafla hiyo Mgeni maalum, BW. JUMA BWANDO amewataka askari Polisi kuendelea kusimamia majukumu ya kwa kadiri ya miongozo na taratibu za Jeshi hilo, na kuendelea kulitumikia kwa uaminifu mkubwa.
END.
M4C
Ben Komba/Pwani-Tanzania/10-Feb-13/13:42:54
Chama cha demokrasia na maendeleo kimewataka wananchi kutokubali kurubuniwa kwa kuwaambia CHADEMA ni chama cha kidini kunakosababishwa kwa baadhi ya vyama kutumia propaganda hiyo kutaka kuwagawa watanzania na baadaye kuwatawala kwa kufuata mifumo ya kurithishana kama inavyojidhihirisha hivi sasa.
Akiongea katika mkutano wa vuguvugu la mabadiliko inayoendelea nchi hivi sasakatika viwanja vya stendi ya Mzenga katika mamlaka ya mji mdogo wa Mlandizi yenye kulenga kutekeleza kauli ya mwaka wa nguvu ya umma inayoeendeshwa na chama cha demokrasia na kufanikiwa kuleta mitazamo chanya kwa wakazi wa wilaya ya Kibaha kutokana na kuwepo piga nikupige ya mikutano kati ya chama cha CHADEMA na CCM.
Kada wa chama cha demokrasia na maendeleo kutoka Arusha, BW.ALLY BANANGA amesema cha cha CCM kimekuwa chama cha kurithisha uongozi na kuyatupa kando malengo ya awali ya uanzishaji wa chama hicho ambayo yalikuwa hayana lengo la kujenga himaya za kisultani kwa baadhi ya viongozi na familia zao kama ilivyo hivi sasa kwa kuzusha mambo ambayo hayana ukweli wowote katika kujaribu kuwagawa watanzania kiimani.
BW. BANANGA amebainisha kumekuwepo na harakati kubwa katika kuhakikisha wanafanikiwa kukamata dola mwaka 2015 na kuwaasa wana Kibaha ambo wamechoka kunyanyaswa na kukandamizwa na chama tawala kuunga mkono harakati hizo za CHADEMA zenye lengo la kumkomboa mtanzania na mgogoro mkubwa wa kimfumo tunaokabiliana nao kutokana na baadhi ya watu kujiona kama wana hati miliki na Taifa hili.
END.
Comments
Post a Comment