OPERESHENI SENSA 2012.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/21 February, 2013/15:59:31
Kikosi namba 832 cha Jeshi la kujenga Taifa Ruvu, kimetoa wahitimu 994 wa mafunzo ya awali ya kijeshi ya vijana maarufu kama operesheni sensa 2012 ikiwa ni mhafali ya 102 tangu kuanzishwa kwa Jeshi hilo ambapo kati ya wahitimu hao wavulana ni 754 na wasichana 240.
Kwa mujibu wa risala iliyosomwa na mmoja wa wahitimu hao AFANDE. MARTIN MABENA, inasema kuna baadhi ya hao vijana walioshiriki mafunzo hayo ya opersheni sensa kuna walioshindwa kuhitimu mafunzo hayo kutokana na sababu za kiafya ni mmoja, vifo wawili, utovu wa nidhamu wawili na kuwa na jumla ya wahitimu watano walioshindwa kuhitimu mafunzo hayo kati yao wavulana wakiwa wawili na wasichana watatu.
AFANDE MABENA amesema katika risala hiyo kuwa malengo ya operesheni sensa ni kujenga uzalendo na uvumilivu miongoni mwa vijana wa Tanzania, ikiwa pamoja na kuwaanda kuwa raia wema ili kuwezesha upatikanaji wa viongozi bora watakaoweza kuiilinda nchi na kuitumikia kwa malengo ya kujenga umoja wa kitaifa sawa na kuwajengea viajana uwezo wa kujiajiri.
Risala hiyo iliyosomwa na AFANDE. MARTIN MABENA imebainisha kuwepo kwa changamoto mbalimbali ambazo wamekabiliana nazo katika kipindi cha mafunzo ya operesheni sensa lakini wameainisha mafanikio mbalimbali waliyopata ikiwa pamoja na kufufua shamba la mpunga lenye ukubwa hekari zisizopungua 500 ambalo lilikuwa pori kwa kipindi cha miaka 19 niliyopita, ikiwa na kukarabati eneo la fatiki ya kikwazo.
Akifunga mafunzo hayo Mkurugenzi wa SUMA JKT, BRIGEDIA JENERALI MWANAMAKALA MOHAMED KILLO amebainisha kuwa tukio hilo ni kubwa kitaifa ikiwa ni katika kuwapa majukumu makuu mawili moja ni katika kulinda Taifa lao na kuwapatia mafunzo ya ujasiriamali.
Na hasa amevutiwa na zoezi ambalo wamelifanya la kukarabati vikwazo na kumwonyeshauwezo wa kuvitumia na hasa ukizingatia vikwazo ndio kitu muhimu katika Jeshi katika kumjenga askari kuwa mkakamavu.
END.
Comments
Post a Comment