NHIF - PWANI
NHIF PWANI
Ben Komba/Pwani-Tanzania/08-Feb-13/8:09:28
Mfuko wa Bima ya afya katika mkoa wa Pwani umewataka wadau wa mfuko huo kufanya kazi za utoaji huduma za mfuko huo kwa kushirikiana na kutimiza wajibu kwa kila mtu na eneo lake ili kukabiliana na chnagamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo katika uendeshaji wa mfuko huo.
Meneja wa mfuko wa Bima ya afya katika mkoa wa Pwani, BW. ANDREW MWILUNGU amesema kuwa ofisi ya mkoa wa Pwani imezinduliwa rasmi Oktoba 3, 2002 na toka kuanzishwa kwake wamekuwa wakifanya kazi karibu na waandishi katika kuhakikisha wananchi wanapata taarifa za kutosha kuhusiana na mfuko huo.
BW. MWILUNGU amebainisha kuwa ufanisi katika mkoa wa Pwani umeongezeka kutokana na sasa kuwepo na usimamizi wa karibu wa utekelezaji wa malengo ya mfuko huo kwa kusimamia kwa karibu wadau wengine ambao wanahusika katika zoezi zima la kutoa huduma kupitia mfuko huo.
Meneja huyo wa Mfuko wa Bima ya afya katika mkoa wa Pwani, BW. ANDREW MWILUNGU amebainisha kuwa kwa sasa wao wana jukumu la kusimamia na mfuko wa fya ya jamii katika kuhakikisha huduma za mifuko ya afya zinafanyika kwa ufanisi na kiwango kinachostahili katika suala zima la kuhakikisha mteja anapata huduma stahili kwa kadiri ya makubaliano.
Naye Ofisa uhusiano mwandamizi wa mfuko wa Bima ya afya, BW. LUHENDE SINGU amesema katika kuhakikisha kila mtu anapata dawa na kusisitiza asilimia 67 ya fedha za uchangiaji wa huduma zirudishwe kwa ajili ya matumizi ya kununulia dawa, na mara nyingi ofisi ya mkurugenzi imekuwa ikizorota katika kusimamia fedha za mfuko wa Bima ya afya kwa kutumia fedha husika kwa matumizi tofauti.
BW. SINGU amewaomba waandishi wa habari kusaidia kuielimisha jamii kuhusu faida ya kujiunga na mfuko wa Bima ya afya, kwa kukanusha kwamba eti mahospitalini hakuna dawa hata kama utajiunga na mfuko huo kitu ambacho si kweli bali ni uzembe wa baadhi wa watumishi wa zahanati/hospitali na maduka ya dawa kwa sababu zao binafsi.
END.
Comments
Post a Comment