MAJI CHANZO KIBAHA WANAOFAIDIKA NI WA DAR ES SAALAM.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/16-Feb-13/20:23:45
Kukosekana kwa maji ya bomba kwa takriban mwezi mmoja kumesababisha Diwani wa Kata ya Mailimoja mjini Kibaha BW. ANDREW LUGANO kufanya ziara ya ghafla katika ofisi ya DAWASCO katika mkoa wa Pwani kutaka kujua ni nini chanzo cha ukosefu wa maji katika mji huo ili hali chanzo kipo mkoani mwao.
Katika Ofisi za DAWSCO tulibahatika kumkuta Meneja wa DAWASCO, BW. ROBERT MUGABE ambaye baada ya kuelezwa kuhusu tatizo hilo ukapita uamuzi wa meneja huyo ambaye alidai maji jana yake yalitoka kuambatana na diwani huyo kwenda kumuonyesha maeneo ambayo maji kwao sasa ni kitendawili.
Baadhi ya maeneo ambayo yalifikiwa na Meneja huyo wa DAWASCO kushuhudia mwenyewe kutokuwepo maji na uhariobifun wa miundo mbinu ambayo DAWASCO wamezembea kufanya ukarabati na wakijua kutofanya hivyo ni kusababisha wateja kukosa huduma hiyo muhimu kwa binadamu.
Baadhi ya wananchi wameelezea kukerwa kwao na wasoma mita ambao wamekuwa wakifika majumbani kwao ilihali wakijua maeneo yao hawapati maji kitu ambacho kinawasababishia hasira, na kuwataka DAWASCO kutumia gari la matangazo wakati wanapotaka kukata maji kama wanavyofanya operesheni ya kukata maji zaidi fuatilia ziara hiyo...
END.
Comments
Post a Comment