UWT KTA YA TUMBI YATOA MSAADA KWA WAGONJWA.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/02-Feb-13/17:38:00
Jumuiya ya wanwake wa chama cha mapinduzi wametembelea hospitali Maalum ya rufaa ya Tumbi iliyopo mjini Kibaha katika mkoa wa Pwani, ambapo walitumia fursa hiyo kutoa msaada wa kiutu kwa wagonjwa ambao wamelazwa katika wodi ya watoto na kufanya usafi kuzunguka maeneo ya hospitali.
Mwenyekit wa jumuiya ya wanawake kata ya Tumbi, BIBI. CLEMENTINA NGONYANI amesema tukio hilo nim maadhimisho a miaka 36 ya kuzaliwa kwa chama hicho, ambapo kilele chake ni siku ya Jumapili Februari kimkoa na maadhimisho yake yatafanyika Utete wilayani Rufiji ambapo wageni mbali mbali wameshaelekea huko.
BIBI. NGONYANI amebainisha kwa kufanya hivyo kutasidia kukiweka chama hicho karibu na wananchi na kuweza kuwaelekeza kuwa CCM ndio chama imara ambacho kitaweza kuwakomboa wananchi kutoka katika hali duni mpaka kufikia matarajio yao wakipea nafasi zaidi.
Katibu wa Jumuiya ya wanawake katika Kata ya Tumbi, BIBI GENOVEVA JEREMIAH amesema wameamua kuadhimisha kuaadhimisha miaka 36 ya kuzaliwa kwa CCM kwa kufika hospitali ya Tumbi kuona wagonjwa na kutoa msaada ya nkiutu kwa wagonjwa sawa na kufanya usafi.
BIBI. JEREMIAH amevitaka vyama vingine kufanya hivyo badala ya kukaa na kuibeza CCM, na kata ya Tumbi imeonyesha mfano kuwa CCM inaweza na kuwajali wananchi wanowatawala.
Mjumbe wa Baraza la UWT katika mkoa wa Pwani aambaye naye ameshiriki zoezi hilo, BIBI. ASNATH JEREMIAH GERVAS amesema kuwa kutokana na jisia yao kuwa wanawake wameona vyema waweze kufika hospitalini hapo ili kuja kuwasaidia wanawake wenzao, na ikichukuliwa kuwa ni siku maalum ya wakiwa wwanaelekea katika maadhimisho ya miaka 36 ya CCM.
Msaada ambao umetolewa na Jumuiya hiyo ya wanawake wa CCM Kata ya Tumbi ni pamoja na sabuni na biscuti ikiwa pamoja na kufanya usafi na kuwafariji wagonjwa mabao wamelazwa katika hospitali hiyo ya maalum ya rufaa ya Tumbi katika wodi ya watoto.
END.
Comments
Post a Comment