MAHABUSU WAPATA BASI LA KUWABEBA PWANI.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/01-Feb-13/8:47:00
Jukumu la kusafirisha mahabusu kutoka wanakoshikiliwa kupelekwa mahakamani mjini Kibaha limekabidhiwa rasmi kwa Jeshi la magereza katika suala zima la kuleta mabadiliko ya kiutendaji katika idara mbili hizo za serikali.
Mwandishi wa habari hizi ameshuhudia Basi la kubeba Mahabusu likiwa eneo la mahakama ya Mkoa wa Pwani, kufuatia uzinduzi uliofanyika katika gereza la Ubena na kuzinduliwa rasmi na Naibu waziri wa Mambo ya ndani, BW. PERREIRA AME SILIMA na kushuhudia na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa.
Mkoa wa Pwani ni mmoja wa wa mikoa ambayo imezindua utaratibu huo ambao kwa sasa utahakikisha usalama wa mahabusu na askari kutokana na kupata basi hilo maalum kwa ajili ya kazi ya kubeba mahabusu, tofauti na awali ambapo walikuwa wakipakizwa katika LAND ROVER na kufanya askari kulazimika kuning'inia huku akiwa ameshika bunduki, hali ambayo ilisababisha baadhiu ya wafungwa kutoroka.
Baadhi ya mikoa amabayo tayari imeshaanzisha utaratibu huo ni Dar e saalam, Arusha, Mwanza, Dodoma ambao wao wameanza takriban mwaka 1 uliopita, Chanzo cha habari hizi ambacho kimekataa kutajwa jina lake amebinisha kwa kufanya hivyo kutaimarisha haki za binadamu kwa mahabusu na kupunguzia vituo vya Polisi mzigo wa kulaza mahabusu kwa siku 14 ilihali kituo kikiwa hakina huduma za kulaza mahabusu.
Chanzo kimebainisha mtuhumiwa anatakiwa kukaa Kituo cha Polisi sio zaidi ya masaa 24, na kwa upande wa Jeshi la Polisi wao watapata nafuu ya kufanya kazi katika mazingira magumu kutokana na kukosa usafiri wa kusafirisha mahabusu kutoka mahabusu kwenda mahakamani.
Ruti za basi hilo ambalo linaonekana madhubuti kutokana na jinsi lilivyotengenezwa litaanza ruti zake mahabusu ya SEGEREA, MKUZA, UBENA na KIGONGONI na kuwashusha mahabusu hao sehemu ambazo zitawajibika kusoma kesi zao.
END.
Comments
Post a Comment