TANZANIA COALITION ON DEBT AND DEVELOPMENT.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/13/02/11/17:40:47 Mtandao unaojishughulisha na madeni na maendeleo nchini umepongeza wilaya ya Kibaha kwa kuweza kuwashawishi watoto wa wa kike kujiendeleza kielimu ikiwa pamoja na kuwepo na ahueni katika uwiano unaoridhisha kati ya walimu na wanafunzi ambapo kwa sasa mwalimu mmoja anafundisha watoto 35 kulinganisha na maeneo mengine Mkurugenzi wa mtandao wa madeni na maendeleo nchini, BW. HEBRON MWAKAGENDA ametoa pongezi hizo kwa halmashauri zote mbili za wilaya ya Kibaha wakati wa kuwasilisha ripoti ya utafiti kuhusiana na hali ya elimu na afya kwa wilaya kadhaa nchini, kwa kuweza angalau kukabiliana na mapungufu mbalimbali ikiwa pamoja na kuweka mazingira mazuri ya utoaji na upatakanaji wa huduma ya elimu. BW. MWAKAGENDA amebainisha kuwa sekta ya elimu ni ni moja ya vipaumbele muhimu katia utekelezaji wa mpango mzima wa MKUKUTA ikiwa ni nguzo mojawapo ya kuboresha maisha ya jamii kwa ujumla, utafiti wao wameufanya katika wilaya saba za Morogoro, Kibaha, Kiteto, Lindi, Masasi na Mbarali, na utafiti huo ulishirikisha shule za kata 65. Mkurugenzi huyo wa TCDD, BW. MWAKAGENDA amebainisha kuwa katika utafiti wao wamegundua ongezeka la idadi ya wanafunzi katika shule za sekondari, uwiano kati ya idadi ya wanafunzi na walimu, mazingira ya kufundisha na kujifunzia, idadi ya watoto wanaoacha shule na sababu zake, miundombinu na bajeti katika elimu. Katika utafiti wao wamegundua kuwa kuna ongezeko kubwa la wanafunzi wanaoacha shule katika wilaya zilizofanyiwa utafiti, na wilaya iliyoonyesha ongezeko kubwa la wanafunzi wanaoacha shule ni Iramba ambayuo katika mwaka 2009 ilikuwa na wanafunzi 2457 ambao wameacha shule na katika mwaka 2010 ni walioacha shuleni 2611. END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA