KAMPENI YA MAMA MISITU RUVU KUSINI.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/05-Feb-13/02:47:28 PM Mpango wa Mama misitu wenye lengo la kuhifadhi misitu ya asili katika msitu wa Ruvu kusini katika wilaya za Kibaha na Kisarawe, umeingia awamu ya pili ambayo italenga katika kuwajengea uwezo viongozi katika ngazi mbalimbali kuweza kulinda na kuisimamia misitu kwa umakini. Mratibu wa Mama Misitu katika msitu wa Ruvu kusini, BW. YAHYA MTONDA amesema kwa upande wa wananchi mpango huo umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani wakazi wa vijiji kumi vya majaribio wananchi wamepata mwamko wa kutosha kuhusiana na utunzaji wa misitu katika eneo hilo la Ruvu Kusini. BW. MTONDA amebainisha kwa sasa wanatgegemea kuwafikia viongozi wa kata na wilaya ili kuwapatia elimu zaidi juu ya umuhimu wa kulinda misitu ya asili kama ilivyofanyika kwa wananchi ambao kwa sasa wenyewe wamefikia hatua ya kufanya doria katika msitu wa Ruvu kusini, ikiwa pamoja na kutoa taarifa wanapoona uharibifu wowote unafanyika. Amesema kampeni ya mama msitu kampeni inafanya kazi katika vijiji kumi mara baada ya kuzinduliwa Agosti mwaka jana, kwa upande wa wilaya ya Kibaha kuna vijiji vinne vya BOKO MNEMELA, SOGA, MPIJI, KIPANGEGE na upande wa wilaya ya Kisarawe ni vijiji vya Kibwemwenda, Kola, Malangalanga, Kifuru, Kisanga, Chakenge, Mtamba. BW. YAHYA MTONDA Mratibu wa mradi wa mama misitu katika msitu wa Ruvu kusini akieleza mikakati mbalimbali ambayo inalenga katika utunzaji wa misitu ya asili kwa kushirikisha jamii inayozunguka msitu wa Ruvu kusini ambapo lengo kubwa ni kuwezesha jamii kutambua umuhimu wa hifadhi wa misitu. Baada ya kukamilisha mwaka jana kampeni ya mama misitu,BW. MTONDA amebainisha mipango ya baadaye ni kukutana na mkuu wa wilaya na kamati ya uvunaji ili kuwekana sawa katika suala la uhifadhi wa misitu asilia, ikiwa na uimarishaji wa doria katika maeneo yanayozunguka msitu wa Ruvu Kusini kwa kuongeza elimu juu ya uhamasishaji juu ya suala hilo. END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA