VIDEO - CWT WACHAGUANA PWANI.
Ben Komba
/Pwani-Tanzania/4/25/2015 11:28:27 PM
Chama cha
Walimu mkoa wa Pwani Kimefanya uchaguzi wake mkuu wa kuchagua viongozi
watakawaongoza katika kipindi kijacho cha uongozi katika uchaguzi uliofanyika
mjini Kibaha.
Akizungumza
na waandishi wa Habari ofisini kwake K
atibu wa CWT mkoa wa Pwani, BW.NEHEMIAH JOSEPH amesema uchaguzi huo ulikuwa
huru na haki na wajumbe wamefanikiwa kutumia nafasi kuwapata viongozi ambao
watawaongoza teanaa katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
BW.NAHEMIAH
amewataja washindi katika nafasi ya Mwenyekiti wa CWT mkoa wa Pwani
imechukuliwa na BW.JOHN KIRUMBI waakati BI.STELLA KIYABO amepata na ujumbe a
kamati ya utendaji ya CWT, nafasi ya mweka hazina ikichukuliwa na BW.ABOUBAKAR
ALAWI.
Nafasi
Nyingine Zilizogombaniwa Katika uchaguzi huo kwa mujibu wa Katibu wa CWT mkoa
wa Pwaani BW. NEHEMIAH JOSEPH ni pamoja na mjumbe atakayewakilisha CWT,Baraza
la TUCTA ambapo BW.RAJAB NGAMBAGE alishinda na upande mwakilishi katika mkutano mkuu wa TUCTA
nafasi hiyo imechukuliwa na BI. GRACE KALINGA.
END.
Comments
Post a Comment