CHADEMA YAWAPOKA WANACHAMA CCM
Ben
Komba/Pwani –Tanzania/4/11/2015 11:59:27 PM
Chama cha demokrasia
na maendeleo-CHADEMA-katika Kata ya Vigwaza Tarafa ya Msoga wilyani Bgamoyo
kimefanikiwa kumtwaa Katibu wa tawi la
CCM Ruvu Drajani katika hatua ya kujiimarisha kisiasa katika kata hiyo.
Afisa wa
kanda yaw a Chama hicho,BW. JERRY KERENGE ametanabaisha kuwa chama chao
kinaamini katika mtaji, ambao mtaji mkubwa wa kisiasa ni kupata wanachama wengi
iwezekanavyo ili kuweza kufikia malengo.
BW.KERENGE
ameongeza katika kulitambua hilo chama kimepanga kufanya ziara kata nzima ya
Vigwaza ili kutoa elim u ya uraia katika kuwasaidia wananchi nkutambua nafasi
yao katika utawala wan chi.
Ameongeza Afsa
huyo wa Kanda, BW.JERRY KERENGE amewasisitiza wanachama wa chama hicho kuwa na
utulivu kuelekea katika kushika dola hapo itakapofika Oktoba mwaka huu.
Naye aliyekuwa
Katibu wa tawi la CCM Ruvu darajani na kuamua kujiunga na CHADEMA, BW.MOHAMED
PAZI amesema yeye ameamua kujiunga na chama hicho sambamba na Baba yake ni
kutokana na sera zake ambazo zina kila dalili ya kumtakia mema mtanzanaia
kulingfanisha na vyama vingi.
END.
Comments
Post a Comment