MAANDALIZI YA MEI MOSI PWANI YANAENDELEA VIZURI.
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/4/28/2015 9:13:45 PM
Kamati ya
maandalizi ya sikukuu ya MEI MOSI katika mkoa wa Pwani imendelea kuhakikisha
shere hizo zinafana mkoani hapa ambapo kimkoa zinafanyika wilayani Mafia.
Mwenyekiti
wa TUCTA mkoa wa Pwani, BW.PAUL MSILU amesema mpaka sasa wenzao walio katika
wilaya mwenyeji wameletea mchango na waao wanaendelea kuchangia ili kuweza
kufanikisha sherehe hizo zinazotoa fursa kwa wafanyakazi bora kupatiwa tuzo
katika suala zima la kujenga ari ya uwajibikaji.
BW. MSILU
amebainisha kuwa katika maandalizi ya sherehe hiyo wamekuwa wakikabiliwa na
changamoto wa ufinyu wa michango, lakini hata hivyo jitihada zinaendelea katika
kuhakikisha sherehe hizo zinafanikiwa.
Naye mjumbe
wa kamati ya maandalizi Kaimu Katibu wa CHODAWU,
BW.AMIN MSHANGA amesema kwa upande wao wamejiandaa vizuri na kitu wanachoomba
waajiri kuchukua hatua ya kuwasafirisha wafanyakazi katika kuwawezesha
kuhudhuria sherehe hizo.
BW. MSHANGA
ameongeza kuwa katika wilaya Mafia wanachama wao ambao wapo katika maeno ya
hifadhi ya kumbukumbu na mahoteli hivyo kwa kutoa kipaumbele kwa wafanyakazi wa
sekta hiyo katika kuhakikisha haki za wafanyakazi zinazingatiwa.
Comments
Post a Comment