VIDEO-MCHANGE KUGOMBEA U BUNGE KIBAHA MJINI KUPITIA ACT wazalendo.
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/4/11/2015 10:53:35 PM
Uongozi Wa
Kijiji cha Kitonga kata ya Vigwaza Tarafa ya Msoga wilayani Bagamoyo umelaumiwa
kwa kushindwa kufuatilia masuala ya maendeleo ya wananchi na hivyo
kuwasababishia dhiki kubwa wakazi wao.
Mkazi wa
kijiji hicho, BW. ABDUL BAKAR MPONDA amesema hali ya maji ni mbaya katika
kijiji kufuatia mkandarasi aliyepewa kazi ya kusambaza maji katika kijiji hicho
kuondoa bomba awali ambalo lilikuwa kubwa na kuwawekea bomba dogo.
BW.MPONDA
amefafanua kuwa wananchi wa Kitonga ambao wanapakana na mto Ruvu kwa umbali Fulani
imewapasa kutembea umbali mrefu kutafuta huduma hiyo muhimu kwa binadamu.
Aidha ameongeza
kuwa kwa sasa ili kupata huduma hiyo inawapasa kutumia shilingi kati ya 500 na
2000 kwa ajili ya huduma hiyo ilihali wenyewe wanaishi maisha ambayo
yanakabiliwa na changamoto nyingi.
Naye mwanadada
REGINA SIMON amesema maji ni changamoto kubwa kwa maisha yao ya kila siku, na
hivyo kusababisha hali mbaya kwa wananchi hao ambao wengi wao ni watu wenye
kipato cha chini na hivyokuwawia vigumu
wao kupata fedha za kununua maji na fedha ya kula.
BI.REGINA amewataka viongozi wa kijiji hicho
kulifanyia kazi suala hilo ili kuwapatia nafuu wananchi na kuacha kufanya mambo
ya ulaghai ya kuwaahidi wananchi kuwatumikia kwa uadilifu wanapotaka nyadhifa Fulani
na wanapopata wanafanya mambo tofauti.
Mjumbe wa
Kamati ya maji ya kijiji cha Kidogozero, BW.MUSHI amesema kuwa kamati yao
imekuwa iikibanwa na mkandarasi anayeutekeleza kwa kudai hawataki kuingiliwa katika
utekelezaji wa mradi na ndio matokeo yake ni pamoja na kufanya vitu ambavyo
vinaathiri wananchi kwa kushirikiana na baadhi ya watumishi wa halmashauri wanaomkumbatia mtaalamu
huyo ambaye amekuwa akipewa zabuni mbalimbali na kuboronga na huku akiendelea
kupatiwa kazi na halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo.
END.
Comments
Post a Comment