SERIKALI YATAKIWA KUTOA KIPAUMBELE TIBA ASILIA.
Ben Komba
Pwani-Tanzania/4/22/2015 7:16:17 PM
Serikali
imetakiwa kutoa kipaumbele kwa waganga wa tiba za jadi katika suala zima la
kupambana na magonjwa sugu ambayo yanakosa tiba siku hadi siku wakati kuna dawa
za jadi zenye kuweza kupambana na magonjwa hayo.
Mganga BW.ABDALLAH
ATHUMAN MPEMBENWE anayefanya shughuli zake katika kijiji cha Kitonga wilayani
Bagamoyo amesema Tiba za jadi zikipewa kipaumbele na serikali na kuaachana na
dhana waliyokuja nayo wakolono kuwa kila kitu cha mtu mweusi ni cha Kishenzi na
kufanikiwa kuua kwa kiasi kikubwa sayansi ya tiba za asili.
BW.MPEMBENWE
amebainisha kuwa magonjwa kama upofu wa mtu kutoona toka kuzaliwa au kukoma
kuona ghafla kwake yeye si tatizo, kwani mpaka sasa kashatoa tiba kwa wagonjwa
mbalimbali na wengine kushuhudiwa na mwandishi wa Habari hizi.
Hivyo ameitaka
serikali kutupia macho bila kusita upande wa tiba asilia ili nkuweza kuwa na
Taifa la Watu wenye afya na wakakamavu ambao wataweza kulitumikia Taifa lao kwa
mafanikio makubwa na kupunguza idadi ya vifo vya lazima toka nchi yetu
imejaliwa miti dawa ya kutosha kukidhi
mahitaji itakapotakiwa.
Naye kijana ABDALLAH
RAMADHAN wa miaka 17 mhitimu wa darasaa la saba ambaye ameamua kujifunza mambo
ya tiba asilia, BW.MDOGO amesema ameshawishika na uganga wa Tiba asilia baada
ya kushuhudia mjomba wake ambaye alipata upofu wa ghaafla akipona macho kupitia
tiba za asili.
BW. RAMADHAN
akaongeza kuwa hali hiyo ilimsukuma nay eye kutaka kujifunza masuala ya tiba za
asilia ili aweze kuwasaidia wananchi wengine watakaokuwa na matatizo.
END.
Comments
Post a Comment