MASHINDANO YA KOMBE LA KOKA YAANZA.
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/4/26/2015 10:13:32 PM
Mashindano ya
kombe la KOKA CUP yamezinduliwa rasmi na Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini,
SILVESTRY KOKA katika viwanja vya Shirika la Elimu Kibaha kwa kuwaasa vijana
kushiriki katika michezo ili kuwa wakakamavu.
KOKA amesema
kuwa suala la vijan kushiriki michezo ni suala la msingi na hivyo amewataka
vijana hao kutmia mashindano hayo ya mpira wa miguu kuendeleza vipaji vyao na
hasa ikizingatiwa michezo ni burudani na ajira.
Aidha ameongeza
kuwa mashindano hayo ni jitihada ya kuenzi michezo ili kuwa na wachezaji mahiri
ambao watakwenda kuunda timu ya Jimbo ambayo itapatikana kwa kuchagua wachezaji
wenye uwezo wa kusakata kabumbu ili kujenga timu bora ambayo itakuwa mfano.
END.
Comments
Post a Comment