CHADEMA YAPOKA WANACHAMA WA CCM BAGAMOYO



Ben Komba/Pwani –Tanzania/4/11/2015 11:59:27 PM
Chama cha demokrasia na maendeleo-CHADEMA-katika Kata ya Vigwaza Tarafa ya Msoga wilyani Bgamoyo kimefanikiwa kumtwaa Katibu wa    tawi la CCM Ruvu Drajani katika hatua ya kujiimarisha kisiasa katika kata hiyo.

Afisa wa kanda yaw a Chama hicho,BW. JERRY KERENGE ametanabaisha kuwa chama chao kinaamini katika mtaji, ambao mtaji mkubwa wa kisiasa ni kupata wanachama wengi iwezekanavyo ili kuweza kufikia malengo.

BW.KERENGE ameongeza katika kulitambua hilo chama kimepanga kufanya ziara kata nzima ya Vigwaza ili kutoa elim u ya uraia katika kuwasaidia wananchi nkutambua nafasi yao katika utawala wan chi.

Ameongeza Afsa huyo wa Kanda, BW.JERRY KERENGE amewasisitiza wanachama wa chama hicho kuwa na utulivu kuelekea katika kushika dola hapo itakapofika Oktoba mwaka huu.

Naye aliyekuwa Katibu wa tawi la CCM Ruvu darajani na kuamua kujiunga na CHADEMA, BW.MOHAMED PAZI amesema yeye ameamua kujiunga na chama hicho sambamba na Baba yake ni kutokana na sera zake ambazo zina kila dalili ya kumtakia mema mtanzanaia kulingfanisha na vyama vingi.


END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA