VIDEO-MGOMO WA MABASI WAATHIRI SHUGHULI ZA MAENDELEO.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/4/10/2015 7:22:20 PM
Mgomo mkubwa
wa mabasi ya kubeba abiria kutoka Mkoa
wa Dar es Saalam kuelekea mikoa mbalimbali ya Tanzania umefanyika na kuathiri
kwa kiasi kikubwa shughuli mbalimbali za maendeleo.
Abiria wengi
wameonekana katika stendi ya mabasi ya Mailimoja wengi wao kutoka mikoa ya
Mwanza na Kagera ambao hulazimika kulala njiani na kuwapasa kusafiri kwa siku
mbili kufatia utaratibu mpya ambao umewekwa na serikali.
Nimdebahatika
kuongea na wafanyakazi hao wa mabasi ya kusafirisha abiria, abiria na viongozi
wa mawakala wa mabasi yanayosafirisha abiria katika kituo cha mabasi cha
Mailimoja.
Zaidi fuatilia
hali halisi ya sakata zima la mgomo ambao umendeshwa na madereva nchi nzima
kupinga kulazimishwa kurudfi shule ya mafunzo ya kazi hiyo kila baada ya miaka
mitano ya kuhalalisha tena leseni yake kwa ada ya shilingi zzaidi ya shilingi
laki tano, kitu ambacho madereva hawakubaliani nacho.
END.
Comments
Post a Comment