VIDEO-SERIKALI YATAKIWA KUHESHIMU TIBA ASILIA.

Ben Komba Pwani-Tanzania/4/22/2015 7:16:17 PM
Serikali imetakiwa kutoa kipaumbele kwa waganga wa tiba za jadi katika suala zima la kupambana na magonjwa sugu ambayo yanakosa tiba siku hadi siku wakati kuna dawa za jadi zenye kuweza kupambana na magonjwa hayo.
Mganga BW.ABDALLAH ATHUMAN MPEMBENWE anayefanya shughuli zake katika kijiji cha Kitonga wilayani Bagamoyo amesema Tiba za jadi zikipewa kipaumbele na serikali na kuaachana na dhana waliyokuja nayo wakolono kuwa kila kitu cha mtu mweusi ni cha Kishenzi na kufanikiwa kuua kwa kiasi kikubwa sayansi ya tiba za asili.

BW.MPEMBENWE amebainisha kuwa magonjwa kama upofu wa mtu kutoona toka kuzaliwa au kukoma kuona ghafla kwake yeye si tatizo, kwani mpaka sasa kashatoa tiba kwa wagonjwa mbalimbali na wengine kushuhudiwa na mwandishi wa Habari hizi.

Hivyo ameitaka serikali kutupia macho bila kusita upande wa tiba asilia ili nkuweza kuwa na Taifa la Watu wenye afya na wakakamavu ambao wataweza kulitumikia Taifa lao kwa mafanikio makubwa na kupunguza idadi ya vifo vya lazima toka nchi yetu imejaliwa miti  dawa ya kutosha kukidhi mahitaji itakapotakiwa.

Naye kijana ABDALLAH RAMADHAN wa miaka 17 mhitimu wa darasaa la saba ambaye ameamua kujifunza mambo ya tiba asilia, BW.MDOGO amesema ameshawishika na uganga wa Tiba asilia baada ya kushuhudia mjomba wake ambaye alipata upofu wa ghaafla akipona macho kupitia tiba za asili.

BW. RAMADHAN akaongeza kuwa hali hiyo ilimsukuma nay eye kutaka kujifunza masuala ya tiba za asilia ili aweze kuwasaidia wananchi wengine watakaokuwa na matatizo.

END. 

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA