WATANZANIA WAONYWA RUSHWA KIPINDI CHA UCHAGUZI


Ben Komba/Pwani-Tanzania/4/17/2015 4:19:28 PM
Watanzania wametakiwa kufanya maamuzi sahihi itakapofika kipindi cha uchaguzi bila ushawishi  wa chapaa ili kuweza kupata viongozi wanaostahili pasipo kutumia rushwa.

Mjumbe halmashauri kuu ya Taifa ya chama cha mapinduzi kutoka Kibaha mjini, BW.RUGEMALIRA RUTATINA wakati akiongea na wanachama wa CCM kutoka Kata ya Mailimoja ambapo amesema rushwa isiwe msingi wa uchaguzi wa CCM.

Bw.RUTATINA amesema inasikitisha kuona baadhi ya watu wanafanya maamuzi kwa shinikizo la rushwa na kujikuta wanachagua kiongozi bila kujali uwajibikaji wake.
Aidha amechukua fursa hiyo kuwaasa Wanaccm kwenda kuisoma katiba pendekezwa sambamba nay a zamani ilii waweze kujua ukweli kuhusiana na suala hilo na hivyo kuweza kujitokeza kupiga kura ya maoni ya katiba kwa kujitambua.

BW.RUTATINA amewasisitiza wanachama wa CCM kujitokeza kwa wingi kwenda kujiandikisha katika daftari la mpiga kura zamu itakapofika.


END. 

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA