VIDEO-MKANDARASI ASABABISHA DHIKI KWA WANANCHI KITONGA BAGAMOYO.
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/4/11/2015 10:53:35 PM
Uongozi
Wa Kijiji cha Kitonga kata ya Vigwaza Tarafa ya Msoga wilayani Bagamoyo
umelaumiwa kwa kushindwa kufuatilia masuala ya maendeleo ya wananchi na hivyo
kuwasababishia dhiki kubwa wakazi wao.
Mkazi
wa kijiji hicho, BW. ABDUL BAKAR MPONDA amesema hali ya maji ni mbaya katika
kijiji kufuatia mkandarasi aliyepewa kazi ya kusambaza maji katika kijiji hicho
kuondoa bomba awali ambalo lilikuwa kubwa na kuwawekea bomba dogo.
BW.MPONDA
amefafanua kuwa wananchi wa Kitonga ambao wanapakana na mto Ruvu kwa umbali
Fulani imewapasa kutembea umbali mrefu kutafuta huduma hiyo muhimu kwa
binadamu.
Aidha
ameongeza kuwa kwa sasa ili kupata huduma hiyo inawapasa kutumia shilingi kati
ya 500 na 2000 kwa ajili ya huduma hiyo ilihali wenyewe wanaishi maisha ambayo
yanakabiliwa na changamoto nyingi.
Naye
mwanadada REGINA SIMON amesema maji ni changamoto kubwa kwa maisha yao ya kila
siku, na hivyo kusababisha hali mbaya kwa wananchi hao ambao wengi wao ni watu
wenye kipato cha chini na hivyokuwawia
vigumu wao kupata fedha za kununua maji na fedha ya kula.
BI.REGINA amewataka viongozi wa kijiji hicho
kulifanyia kazi suala hilo ili kuwapatia nafuu wananchi na kuacha kufanya mambo
ya ulaghai ya kuwaahidi wananchi kuwatumikia kwa uadilifu wanapotaka nyadhifa
Fulani na wanapopata wanafanya mambo tofauti.
Mjumbe
wa Kamati ya maji ya kijiji cha Kidogozero, BW.MUSHI amesema kuwa kamati yao
imekuwa iikibanwa na mkandarasi anayeutekeleza kwa kudai hawataki kuingiliwa
katika utekelezaji wa mradi na ndio matokeo yake ni pamoja na kufanya vitu
ambavyo vinaathiri wananchi kwa kushirikiana na baadhi ya watumishi wa halmashauri wana
END.
Comments
Post a Comment