VIDEO-ZOEZI LA CHANJO KWA WATOTO LAANZA RASMI MJINI KIBAHA.
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/4/24/2015 8:16:16 PM
Halmashauri
ya mji wa Kibaha imeanza utoaji wa chanjo kwa watoto kwa ajili ya kinga ya
magonjwa sumbufu kwa watoto katika kuhakikisha
vifo vya watoto wadogo vinapungua kwa kiasi kikubwa.
Msimamizi wa
huduma ya Mama, Baba na mtoto, BI.JANEROSE JOHN amesema kuwa lengo la chanjo
hiyo ni mpagoa kitaifa wa utoaji wa chanjo kwa watoto wenye umri wa chini ya
miaka mitano katika kupunguza uwezekano wa
kuzui magonjwa yanayoweza kupata kinga.
BI.JOHN
ameongeza magonjwa yanayoweza kukingwa na chanjo hiyo ni kifua
kikuu,kuharisha,Polio,donda koo, kupooza, kifaduro na kichomi, na amesema lengo
la chanjo hiyto ni kutaka kuhakikisha kizazi kijavcho kinakuwa hakisumbuliwi na
magonjwa hayo.
Aidha
ameongeza kuwa wamekuwa wakikabiuliwa na mzigo mkubwa wa wateja kulinganisha na
watum ishi waliopo kutokana na kuwepo na
mwingilianao na Mkoa wa Dar es saalam na
kutaka jamii ielewe wanapoona kuna msongamano wa watu kwani ni njke ya uwezo
kutokana na kituo hicho kuhudumia watu kutka nje ya mkoa wa Pwani.
Mwenyekiti
wa Bodi wa afya ya Halmashauri ya mji wa Kibaha, BW.MBOGO PAUL MBOGO amesema
suala la chanjo ni suala muhimu kwa ustawi wa afya ya mtoto na kujenga Taifa la
watu wenye afya njema.
BW.MBOGO
ameongeza kuwa yeye akiwa madau kutoka jamii amekuwa akitumia muda wake mwingi
kuhamasisha jamii kuzingatia chanjo inayotolewa kwa watoto ili kuwawezehsa
kuwaepusha na magonjwa yanayoweza kuzuilika.
END.
Comments
Post a Comment