ACT-YAANZA VIKAO VYA MKAKATI PWANI.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/4/26/2015
8:44:42 PM
Mjumbe wa
kamati kuu ya Chama cha ACT-ALLIANCE FOR CHANGE AND TRANSPARENCY, BW. HABIB
MCHANGE amewataka Watanzania kukiunga
mkono Chama hicho Kichanga ili kuweza kuwatoa katika lindi la umaskini
unaowakabili.
Mjumbe huyo
wa Kamati kuu ya ACT, BW.MCHANGE amesema kuwa chama hicho ni chama chenye lengo la kuwakomboa wananchi wa
kawaida ikiwza pamoja na kuwapatia fursa watu wa kawaida kuweza kuwa viongozi.
BW.MCHANGE
amefafanua kwamba muundo wa Chama hicho umelenga kutoa nafasi kwa watoto wa
makabwela kwa kupanga safu ya sura mpya kabisa katika masuala tofauti na
ilivyozoeleka katika vyama vingine vya siasa kwa viongozi kurithisha madaraka
bila kujali uwezo wa mrithi.
Naye katibu
wa ACT, BW.MRISHO SWAGALA amefafanua kuwa Chama hicho kichanga kina nia ya
kweli ya kumkomboa Mtanzania na kwa kuanzia amewataka kinamama kujiunga katika
vikundi ili waweze kukopeshwa na kuzisaidia familia zao na sera yao kubwa ni
siasa za ujamaa katika kuwaenzi Waasisi wa Tanzania MWL.JULIUS NYERERE na MZEE
ABEID AMAN KARUME.
END.
Comments
Post a Comment