VIDEO-WA-MAMA WAPONGEZWA KUJIKITA KATIKA UJASIRIAMALI.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/4/17/2015 3:15:50 PM
Wananchi mjini Kibaha wametakiwa kusimama bega kwa bega kuhakikisha wanaendelea kushirikiana katika kujikwamua na hali ngumu ya maisha ili kujiletea uastawi wao wenyewe na familia hizo.

Mbunge wa Kibaha mjini, BW.SILVESTRY KOKA amesema hayo akizungumza na kinamama wa CCM wa Kata ya Tumbi ambapo pia amezindua mashina 10 ya umoja wa wanawake wa CCM na kuwataka kuendeleza juhudi hizo ambazo kwa njia moja au nyingine zilikuwa na uungwaji mkono mkubwa wa Mke wa Mbunge huyo BIBI.SELINA KOKA.

Ambapo Mbunge huyo wa Kibaha mjini, BW.SILVESTRY KOKA amebainisha kuwa toka apate nafasi hiyo yeye na familia yake wametumia zaidi ya shilingi milioni 400 katika kusaidia vikundi mbalimbali vya kijamii katika suala zima la kuwajengea uwezo wa kiuchumi.

BW.KOKA amefurahishwa na matokeo ambayo sasa anayashuhudia kwa kinamama kuwa na mwamko wa mawazo ya uzalishaji mali kama alivyoshuhudia katika ziara yake ya kuzindua mashina ya UWT 16 katika kata ya Tumbi.

Naye Msoma risala kutoka shina UWT namba 13,  SCHOLASTICA MWAIFUGE amesema shina lao lina wanachama hai 30, mashina hayo ni miongoni mwa mashina mapya matatu ya WIPAHS,AIR  MSAE.

BIBI MWAIFUGE ameongeza wakinamama wa shina hilo wanajishughulisha na biashara na ujasiriamali katika kuhakikisha wanafanya shughuli za kiuchumi na kuweza kuzikwamua familia zao kutoka umaskini uliopindukia.

END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA