WA-MAMA WAPONGEZWA KUJITUMBUKIZA KATIKA UJASIRIAMALI.
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/4/17/2015 3:15:50 PM
Wananchi
mjini Kibaha wametakiwa kusimama bega kwa bega kuhakikisha wanaendelea
kushirikiana katika kujikwamua na hali ngumu ya maisha ili kujiletea uastawi
wao wenyewe na familia hizo.
Mbunge wa
Kibaha mjini, BW.SILVESTRY KOKA amesema hayo akizungumza na kinamama wa CCM wa
Kata ya Tumbi ambapo pia amezindua mashina 10 ya umoja wa wanawake wa CCM na
kuwataka kuendeleza juhudi hizo ambazo kwa njia moja au nyingine zilikuwa na
uungwaji mkono mkubwa wa Mke wa Mbunge huyo BIBI.SELINA KOKA.
Ambapo
Mbunge huyo wa Kibaha mjini, BW.SILVESTRY KOKA amebainisha kuwa toka apate
nafasi hiyo yeye na familia yake wametumia zaidi ya shilingi milioni 400 katika
kusaidia vikundi mbalimbali vya kijamii katika suala zima la kuwajengea uwezo
wa kiuchumi.
BW.KOKA
amefurahishwa na matokeo ambayo sasa anayashuhudia kwa kinamama kuwa na mwamko
wa mawazo ya uzalishaji mali kama alivyoshuhudia katika ziara yake ya kuzindua
mashina ya UWT 16 katika kata ya Tumbi.
Naye Msoma
risala kutoka shina UWT namba 13,
SCHOLASTICA MWAIFUGE amesema shina lao lina wanachama hai 30, mashina
hayo ni miongoni mwa mashina mapya matatu ya WIPAHS,AIR MSAE.
BIBI
MWAIFUGE ameongeza wakinamama wa shina hilo wanajishughulisha na biashara na
ujasiriamali katika kuhakikisha wanafanya shughuli za kiuchumi na kuweza
kuzikwamua familia zao kutoka umaskini uliopindukia.
END.
Comments
Post a Comment