VIDEO-WENYE ULEMAVU WAHAMASISHWA KUJITOKEZA KUGOMBEA UCHAGUZI MKUU.
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/4/14/2015 7:37:15 PM
Watu wenye
ulemavu nchini wametakiwa kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu wa madiwani,wabunge na
Rais unaotarajiwa kufanyika Mwezi Oktoba mwaka huu.
Makamu wa
Mwenyekiti wa Chama cha wasioona Tanzania, BW.ROBERT BUNDALA amesema kuwa
wakati umefika kwa watu wenye ulemavu kushiriki kikamilifu katika mchakato wa
kisiasa ili kuweza kupata uwakilishi katika vyombo vya kutoa maamuzi.
Akizungumza katika
ufunguzi wa warsha ya watu wenye ulemavu wa aina tofauti mjini Kibaha,
BW.BUNDALA amewasisitizia washiriki wa warsha hiyto kutokuwa nyuma katika
kuhakikisha na wao washiriki kikamilifu katika mchakato mzima wa uchaguzi mkuu.
Naye mshiriki
wa warsha hiyo, BW.THOMAS MPONDA amewataka Watanzania kuwaunga mkono
wanapojitokeza kugombea nafasi za uongozi badala ya kuwatenga kwa itikadi za
kibaguzi, na alitoa mfano Kata ya Mapinduzi katika Mkoa wa Rukwa ambapo diwani
wa ni mlemavu wa kuona.
BW.MPONDA
amefafanua kutokana na mtazamo hasi uliopo katika jamii ambao hawaamini kama
watu wenye ulemavu wana uwezo wa kuongoza imekuwa changamoto kubwa kwa ulemavu
ikiwa pamoja na miundombinu kukosekana ambayo ingeweza kuwasaidia walemavu.
END.
Comments
Post a Comment