VIDEO-SHULE YA AJABU
Ben Komba/Pwani-Tanzania/4/10/2015
8:10:17 PM
Wakazi wa
kijiji cha Kitonga katika Kata ya Vigwaza wilayani Bagamoyo wamelalamikia
serikali kuhusiana na kufumbia macho kero ya shule ilihali Mbunge wa eneo hil;o
ndiye Waziri anayehusika na elimu, BW.SHUKURU KAWAMBWA.
Mmoja wa
wakazi wa kijiji cha Kitonga wilayani Bagamoyo, BW.AMIR MKEJINA amesema halisi
ya shule ya msingi Kitonga ni ya kusikitisha na ameilaumu serikali kwa kutotoa
kipaumbele kwa shule zilizo pembezoni.
BW.MKEJINA
ameongeza kuwa shule yao ina madarasa saba kamili lakini ikiwa na madarasa
mawili na walimu watano wakiwa na madawati yasiyozidi ishirini katika kipindi
hiki ambacho dunia ipo katika mkipindi cha sayansi na teknolojia.
Mkazi mwingine
wa kijijini hapo Kitonga wilayani Bagamoyo, BW.EMMANUEL MUNGELE amesema yeye
kwa upande wake ameamua kuwahamisha watoto wake kutokana na kwamba watoto
wanamaliza darasa la saba hawawezi kusoma hali ambayo inakatisha tama kwa
wakazi wa kijijini hapo.
Aidha
BW.MUNGELE amesema mbali ya kukabiliwa na tatizo la upungufu wa madarsa na huku
mbunge wa eneo husika akishindwa kusaidia wananchi wa Jimbo lake, suala
barabara kutopitika kipindi cha mvua nalo linabidi livaliwe njuga na serikali
ili kutatua kero hiyo ambayo ipo nje ya uwezo wa wananchi.
Kwani mara
unapofika msimu wa mvua mto Mbiki mdogo ufurika na kukata mawasiliano baina ya
sehemu moja ya kijiji na sehemu nyingine hivyo kufanya wanafunzi kutoenda shule
katika msimu wa mvua kwa kuchelea kusombwa na maji yam to huo.END
Comments
Post a Comment