VIDEO-MEI MOSI PWANI MAMBO MSWANO


Ben Komba/Pwani-Tanzania/4/28/2015 9:13:45 PM
Kamati ya maandalizi ya sikukuu ya MEI MOSI katika mkoa wa Pwani imendelea kuhakikisha shere hizo zinafana mkoani hapa ambapo kimkoa zinafanyika wilayani Mafia.

Mwenyekiti wa TUCTA mkoa wa Pwani, BW.PAUL MSILU amesema mpaka sasa wenzao walio katika wilaya mwenyeji wameletea mchango na waao wanaendelea kuchangia ili kuweza kufanikisha sherehe hizo zinazotoa fursa kwa wafanyakazi bora kupatiwa tuzo katika suala zima la kujenga ari ya uwajibikaji.

BW. MSILU amebainisha kuwa katika maandalizi ya sherehe hiyo wamekuwa wakikabiliwa na changamoto wa ufinyu wa michango, lakini hata hivyo jitihada zinaendelea katika kuhakikisha sherehe hizo zinafanikiwa.

Naye mjumbe wa kamati ya maandalizi Kaimu Katibu wa  CHODAWU, BW.AMIN MSHANGA amesema kwa upande wao wamejiandaa vizuri na kitu wanachoomba waajiri kuchukua hatua ya kuwasafirisha wafanyakazi katika kuwawezesha kuhudhuria sherehe hizo.

BW. MSHANGA ameongeza kuwa katika wilaya Mafia wanachama wao ambao wapo katika maeno ya hifadhi ya kumbukumbu na mahoteli hivyo kwa kutoa kipaumbele kwa wafanyakazi wa sekta hiyo katika kuhakikisha haki za wafanyakazi zinazingatiwa.

END

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA