CHANJO YATOLEWA KWA WATOTO MJINI KIBAHA
Ben Komba/Pwani-Tanzania/4/24/2015
8:16:16 PM
Halmashauri
ya mji wa Kibaha imeanza utoaji wa chanjo kwa watoto kwa ajili ya kinga ya
magonjwa sumbufu kwa watoto katika kuhakikisha
vifo vya watoto wadogo vinapungua kwa kiasi kikubwa.
Msimamizi wa
huduma ya Mama, Baba na mtoto, BI.JANEROSE JOHN amesema kuwa lengo la chanjo
hiyo ni mpagoa kitaifa wa utoaji wa chanjo kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka
mitano katika kupunguza uwezekano wa
kuzui magonjwa yanayoweza kupata kinga.
BI.JOHN
ameongeza magonjwa yanayoweza kukingwa na chanjo hiyo ni kifua kikuu,kuharisha,Polio,donda
koo, kupooza, kifaduro na kichomi, na amesema lengo la chanjo hiyto ni kutaka
kuhakikisha kizazi kijavcho kinakuwa hakisumbuliwi na magonjwa hayo.
Aidha ameongeza
kuwa wamekuwa wakikabiuliwa na mzigo mkubwa wa wateja kulinganisha na watum
ishi waliopo kutokana na kuwepo na
mwingilianao na Mkoa wa Dar es saalam na
kutaka jamii ielewe wanapoona kuna msongamano wa watu kwani ni njke ya uwezo
kutokana na kituo hicho kuhudumia watu kutka nje ya mkoa wa Pwani.
Mwenyekiti wa
Bodi wa afya ya Halmashauri ya mji wa Kibaha, BW.MBOGO PAUL MBOGO amesema suala
la chanjo ni suala muhimu kwa ustawi wa afya ya mtoto na kujenga Taifa la watu
wenye afya njema.
BW.MBOGO ameongeza
kuwa yeye akiwa madau kutoka jamii amekuwa akitumia muda wake mwingi
kuhamasisha jamii kuzingatia chanjo inayotolewa kwa watoto ili kuwawezehsa
kuwaepusha na magonjwa yanayoweza kuzuilika.
END.
Comments
Post a Comment