YAMOTO BENDI KUWASHA MOTO MLANDIZI MEI MOSI.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/4/29/2015 7:59:06 PM
BENDI ya Yamoto inatarajiwa kutoa burudani kwenye mkesha wa siku
ya wafanyakazi Duniani Mei Mosi Aprili 30 mwaka huu kwenye ukumbi wa Container
Bar Mlandizi wilayani Kibaha mkoani Pwani.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa baa hiyo Frank Mwalembwe alisema
kuwa bendi hiyo katika kupamba burudani hiyo itasindikizwa na msanii wa kizazi
Kipya Tunda Man ili kuwapa burudani wakazi wa wilaya hiyo na maeneo jirani.
Mwalembwe amesema kuwa lengo la kutoa burudani hiyo ni kuwaandaa
wafanyakazi katika sherehe yao ambayo inafanyika kila mwaka ambapo kimkoa
itafanyika wilayani Mafia.
Amesema BW. MWALEMBE Burudani hiyo itakuwa ni nzuri kwa wakazi
hao ambapo pia tutaishirikisha bendi ya JKT Ruvu kwa lengo la kutoa burudani
hiyo ambayo itakuwa ya aina yake kwa wakazi wa Mji wa Mlandizi na vitongoji
vyake na vile vya jirani.
Amesema kuwa mbali ya wasanii hao pia kutakuwa na waimbaji
chipukizi wa mkoa wa Pwani nao watapata fursa ya kuonyesha umahiri wao wa
kuimba ili kukonga nyoyo za watu watakaohudhuria shoo hiyo kabambe.
Na ameahidi kuendelea kusaidia wasanii wachanga wa mkoa huu kwa
kuwawezesha ili nao waweze kufikia viwango vya juu kama walivyo wale ambao
tayari wamefanikiwa na kwa kuwawezesha kwa vifaa pamoja na fedha kwa ajili ya
kuinua sanaa kwenye mkoa wa Pwani,
END
Comments
Post a Comment