HABIB MCHANGE KUGOMBEA UBUNGE KIBAHA MJINI KUPITIA ACT WAZALENDO
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/
Chama cha
ACT Mkoa wa Pwani kimeazimia kumsimamisha tena BW.HABIB MCHANGE ambaye uchaguzi
mkuu uliopita aligombea nafasi hiyo kwa tiketi ya Chama cha demokrasia na
maendeleo.
Katibu wa
ACT katika mkoa wa Pwani, BW.MRISHO HALFAN amesema hayo alipoongea na mwandishi
wa Habari hizi kuwa Chma hicho
kimeazimia kumsimamisha BW.MCHANGE kugombea nafasi ya ubunge kupitia chama
hicho.
BW.HALFAN
amefafanua kwamba ana uhakika na mgombea huyo kufanya vizuri katika uchaguzi
ujao kutokana na taarifa zake kujulikana na watu wengi toka alipotoa upinzani
wa kutosha kwa mbunge wa sasa wa Kibaha mjini kupitia tiketi ya CCM.
Akizungumzia
baadhi ya shutuma zinazotolewa na wapiga kura wa Kibaha kuhusiana na kuchukua
rushwa kwa mgombea wao kutoka kwa CCM ili apuuzie kesi ya kupinga matokeo ya
ubunge ya uchaguzi mkuu uiopita ambapo wana Kibaha wapenda mabadiliko walifikia
hatua hata ya kumchangia fedha ili aendeshe kesi hiyo.
Katibu huyo
wa ACT mkoa wa Pwani, MRISHO HALFAN amesema kwanza rushwa haina ushahidi na
BW.MCHANGE hakupewa fedha yoyote kutoka CHADEMA kuendesha zaidi ya shilingi
9000 ambazo alipewa na watu binafsi.
END
Comments
Post a Comment