VIDEO-WAASWA KUTOENDEKEZA RUSHWA YA UCHAGUZI
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/4/17/2015 4:19:28 PM
Watanzania
wametakiwa kufanya maamuzi sahihi itakapofika kipindi cha uchaguzi bila
ushawishi wa chapaa ili kuweza kupata
viongozi wanaostahili pasipo kutumia rushwa.
Mjumbe
halmashauri kuu ya Taifa ya chama cha mapinduzi kutoka Kibaha mjini,
BW.RUGEMALIRA RUTATINA wakati akiongea na wanachama wa CCM kutoka Kata ya
Mailimoja ambapo amesema rushwa isiwe msingi wa uchaguzi wa CCM.
Bw.RUTATINA
amesema inasikitisha kuona baadhi ya watu wanafanya maamuzi kwa shinikizo la
rushwa na kujikuta wanachagua kiongozi bila kujali uwajibikaji wake.
Aidha
amechukua fursa hiyo kuwaasa Wanaccm kwenda kuisoma katiba pendekezwa sambamba
nay a zamani ilii waweze kujua ukweli kuhusiana na suala hilo na hivyo kuweza
kujitokeza kupiga kura ya maoni ya katiba kwa kujitambua.
BW.RUTATINA
amewasisitiza wanachama wa CCM kujitokeza kwa wingi kwenda kujiandikisha katika
daftari la mpiga kura zamu itakapofika.
END.
Comments
Post a Comment