MSIBA WA MWANAMKE KONDAKTA WA DALADALA- VIDEO.
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/3/10/2015
Mamia ya
wakazi wa Kibamba wamekutwa wamekusanyika katika chumba ha kuhifadhia maiti cha
hospitali ya Tumbi katika mkoa wa Pwani, kushuhudia kuagwa kwa mwanadada jasiri
BI.MARY PASCHAL.
Mwanadada
huyo ambaye enzi ya uhai wake alikuwa kondakta wa gari zinazosafirisha abiria
kati ya Ubungo na Kibaha, alipatwa na mauti hayo eneo la Mbezi akiwa kazini
baada gari aina ya NOAH kuigonga HIACE aliyokuwa anafanyia kazi.
Kwa mujibu
wa mashuhuda marehemu katika kipindi hicho alikuwa amekaa katika kiti cha
wanafunzi na huku akiendelea kuita abiria kama ilivyo ada kwa makondakta na
ndipo ilipotokea na kugonga ubavuni gari yao nay eye kudondokea mtarani na
tairi ya nyuma ya gari ikamkanyaga maeneo ya kwenye nyonga
Mwili
marehemu MARY PASCHAL umesafirishwa kwenda WILAYANI Kondoa Mkoani Dodoma kwa
ajili ya mazishi na ameacha watoto wawili mmoja wa darasa la tatu na mwingine
mwanafunzi wa kidato cha pili waliokuwa wanamtegemea.
END.
Comments
Post a Comment