HATIMAYE ILE SHULE MBOVU YAPATA MSAADA-VIDEO.
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/3/9/2015 9:21:20 PM
Mbunge wa
Kibaha mjini,Mheshimiwa SYLVESTER KOKA amekabidhi mabati 50 na mifuko 50 ya
saruji kwa shule ya msingi Maili moja yenye thamani ya shilingi milioni 4 laki 7 katika suala zima la kukabiliana na uchakavu
mkubwa wa majengo uliopo shuleni hapo.
Akikabidhi
msaada huo, Mbunge huyo wa Kibaha mjini, Mheshimiwa KOKA amebainisha kuwa
wakati sasa umefika kuhakikisha kunakuwepo na ushirikiano kati ya walimu na
wazazi ili kuboresha mazingira ya utoaji wa elimu.
Mheshimiwa
KOKA ameongeza kuwa kumlea mwanafunzi si suala la Mwalimu peke yake bali
linahitaji ushirikiano madhubuti kati ya wanafunzi,wazazi na walimu.
Mwalimu mkuu
wa shule ya msingi Mailimoja, BW.REGINALD FANUEL amemshukuru mbunge pamoja na
wadau wengine ambao kwa njia moja au nyingine wamechangia kwa hali na mali
kufanikisha kupatikana vifaa vya ujenzi kwa ajili ya uimarishaji miundo mbinu
ya majengo shuleni hapo.
END.
Comments
Post a Comment