WAKULIMA WA MBOGA WATAKIWA KUTUMIA UMWAGILIAJI WA KUNYUNYIZA, ISRAEL IRRIGATION SYSTEM.
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/3/24/2015 9:36:18 PM
Wakulima wa
mbogamboga nchini wametakiwa kulima kilimo kitakachotumia maji ya wastani ili
kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa maji ya kutosha katika kukidhi mahitaji
ya bidhaa hiyo.
Mtaalamu wa
kilimo cha umwagiliaji kwa kutumia njia ya unyunyuizaji ambayo ni maarufu
nchini Israel inayojulikana kama DRIP IRRIGATION SYSTEM , BW.EPHRAHIM MASSAWE
amesema kwa kufanya hivyo wataweza kukabiliana na changamoto kubwa ya ukosefu
wa maji kwa ajili ya umwagiliaji.
BW.MASSAWE
amebainisha kuwa iwapo wakulima wa mbogamboga watatumia mbinu ya umwagiliaji wa
kunyunyiza wataweza kutumia maji machache wanayopata kwa manufaa na tija kubwa,
kwani mazao yatastawi na kuweza kupata mavuno makubwa.
Mtaalamu huyo
amewasisitizia wakulima wote wa mbogamboga wanaotegemea shughuli hiyo kuendesha
maisha yao ya kila siku kutosita kubadilika na kutumia mbinu mpya za umwagiliaji
ambao utarahisisha upatikanaji wa maji kwani badala ya kutumia maji mengi
kulowesha tuta zima la mboga, teknolojia hiyo nitatoa maji hayo kwenda moja kwa
moja katika mmea husika.
Teknolojia hiyo
ya umwagiliaji imetokea nchini Israel ambapo imetumika na inaendelea kutumika katika
uzalishaji wa kilimo cha matunda katika eneo ambalo awali lilikuwa jangwa.
END.
Comments
Post a Comment