WAANDISHA WANOLEWA TAYARI KWA UCHAGUZI
Ben Komba/Pwani-Tanzania/10/15/2015 6:56:17 AM
Waandishi wa Habari nchini wametakiwa kuhoji baadhi ya Habari mbalimbali zinazotolewa na baadhi ya vyombo vya Habari katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi ambazo zinaweza kusababisha uvinjifu wa amani.
Mwezeshaji katika mafunzo ya waandishi wa Habari ambayo yameandaliwa na BBC MEDIA ACTION kuhusiana na uandishi wa Habari wenye kufuata maadili katika kuripoti Habari za uchaguzi ambayo yamefanyika mjini Dar es Saalam, BW.ATTILIO TAGALILE amesema kuwa vyombo vya Habari vimekuwa vikiripoti kuhusiana na mambo ambayo yanaweza kusababisha vurugu.
BW.TAGALILE ameongeza kuwa kauli kama Goli la mkono au nitachukua nchi mapema asubuhi kwa kauli kama hizo ambazo jamii inazipata kupitia vyombo vya Habari na kutozifanyia kazi ikiwa pamoja na Tume ya uchaguzi na waandishi wa Habari wenyewe kwani walikuwa na wajibu wa kufuatilia ili kupata ufafanuzi jinsi gani wanaweza kutekeleza goli la mkono na vipi itawezekana ushindi mapema asubuhi.
Hivyo amewaasa waandishi wa Habari kueppuyka kuandika Habari kama hizo na hasa ikizingatiwa Jumuiya ya kimataifa inafuatilia kwa karibu mchakato wa uchaguzi mkuu unavyoendelea, na iwapo ikitokea kukatokea vurugu waandishi, chanzo cha maneno hayo basi mahakama ya uhalifu ya kimataifa itawahusu, na kuwasisitizia kuwa makini na kuepuka matatizo kama yaliyomkuta mwandishi wa Kenya, NDG.ARAP SANG.
Naye mshiriki wa mafunzo hayo, BI.SALMA MKALIBALA amewapongeza BBC MEDIA ACTION kwa kuweza kutoa mafunzo hayo ambayo kwa njia moja au nyingine yamemfumbua macho juu umakini kipindi cha kuripoti Habari za uchaguzi ili kuepuka kukiuka maadili ya taaluma.
Mafunzo hayo ambayo yamejumuisha waandishi wa Habari kutoka mikoa ya Lindi, Mtwara, Pwani na Tanga, na yaliandaliwa na BBC MEDIA ACTION na Baraza la Habari Tanzania.
END.
Comments
Post a Comment