VIDEO-MAMA REGINA LOWASSA AKUMBANA NA VURUGU ZIARA YAKE KIBAHA VIJIJINI.
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/10/3/2015 9:07:43 AM
Ujio wa Mama
REGINA LOWASSA katika Jimbo la uchaguzi Kibaha vijijini umekumbwa na vurugu
ambazo kama isingekuwa busara ya wanachama wa CHADEMA basi pangezuka vita.
Kadhia hiyo
imeanza mara baada ya Mama Lowassa kuwasili ofisi ya Jimbo la Chama hicho
Kibaha vijijini kwa ajili ya kutia saini kitabu cha wageni ili baadaye aende
kukagua sehemu alizopangiwa.
Lakini hali
haikuwa rahisi kutoka ofisini hapo baada ya kundi la wanaCCM kutokea na kuziba
barabra ambayo angekuwa aitumie kuondoka ofisini hapo na hivyo kusababisha
kusukumana kwa wananchama wa vyama hivyo viwili.
Huku CCM
wakiongozwa na mchumi wa Jumuiya ya wazazi mkoa wa Pwani, BW.HAJI ABUU JUMA
ambapo walisababisha mtafaruku tosha ambao kama isingekuwa busara ya CHADEMA
basi kampeni zingeingia doa.
END.
Comments
Post a Comment