VIDEO-ACT WAZALENDO WATAKA NEC IWE MACHO NA VITENDO VYA VURUGU KIPINDI CHA KAMPENI.
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/10/5/2015 11:23:20 AM
Chama cha
ACT-WAZALENDO katika mkoa wa Pwani wamekemea tabia ya baadhi ya vyama kufanya
vurugu katika mikutano ya kampeni ya chama chao kama ilivyojitokeza mjini
Kibaha.
Akizungumza
na mwandishi wa Habari hizi, Katibu wa ACT-WAZALENDO mkoa wa Pwani, NDUGU
MRISHO HALFAN amesema kuwa kitendo cha wananchama wa Chama cha CHADEMA kuvamia
kikao cha kampeni cha mgombea ubunge wao na kufanya fujo.
NDUGU HALFAN
ameongeza anashangwaza na tabia za baadhi ya wanachama wa CHADEMA kujitokeza
katika mikutano yao kwa lengo la kufanya vurugu, kitu ambacho amebainisha
hawataweza kuendelea kuvumilia hali hiyo.
Katibu huyo
wa ACT-WAZALENDO ,NDUGU HALFAN ameongeza kwamba ni wajibu wa Jeshi la Polisi
kuhakikisha kuwa linadhibiti vitendo hivyo vinavyoashiria uvunjifu wa amani.
Aidha
ametumia nafasi hiyo kutoa pole kwa wanachama wa chama cha DEMOCRATIC PARTY,
kufuatia kupatwa na msiba wa Mwenyekiti wao, Mchungaji CHRISTOPHER MTIKILA
ambaye amefariki kufuatia ajali ya gari ambayo ilitokea Msolwa wilayani
Bagamoyo.
END.
Comments
Post a Comment