VIDEO-WAISLAMU WAOMBEA AMANI
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/9/6/2015 1:58:44 PM
Waumini wa
dini ya kiislam nchini wamefanya ibada
maalum ya kuombea amani kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani
ambao unatarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.
Mkuu wa
wilaya ya Kibaha, BIBI.HALIMA KIHEMBA kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Pwani,
amesema kuwa viongozi wa dini wana wajibu mkubwa wa kuhakikisha kuwa kunakuwepo
na hali ya amani kabla ya uchaguzi,wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi.
Mkuu huyo wa
wilaya BI.KIHEMBA ameongeza kuwa serikali ina wajibu wa kuhakikisha uchaguzi
unafanyika kwa utulivu,haki na amani, ingawa serikali yenyewe haiwezi bbila
kuwashirikisha wadau ambao ni pamoja na viongozi wa dini katika kuwahimiza
waumini wao kufuata sheria na taratibu zilizopo.
Naye SHEIKH LIPAMBILA MUDHIHIR akielezea
kuhusu uumbaji amesema kuwa Mungu akiombwa anasikiliza, ametoa mfano kuwa Mungu
ameumba binadamu mwanaume na mwanamke, ameumba jua na mvua na mambo mengine
chungu nzima akitaka binadamu wamuogope na kumtukuza.
Amewaasa wanadamu
kujua kuwa kuna Mungu kwa hiyo kitendo cha baadhi yetu kupuuza ibada
kutawagharimu binadamu siku ya amri kiama na amefananisha kuheshimiwa ni kama
mkusanyiko huo kuomba amani na wakiwa hawaelewi maana nzima ya tukio hilo.
Kaimu Mufti
wa Tanzania SHEIKH ABUBAKAR ZUBEIR amesema Watanzania inawabidi kitunza amani
iliyopo kwa hali na mali na hasa kutokana kama amani itavurugika hatutakuwa na
pakukimbilia toka maelfu ya majirani zetu wanamiminika nchini kutokana ukosefu
wa amani katika nchi wananzotoka.
SHEIKH
ZUBEIR amewaasa watanzania kuwa macho na watu ambao wakiona mambo hayaendi kama
wanavyotaka wao uamua kuanzisha vurugu na kuwaacha wanawake,wazee na awatoto
katika dhiki kubwa.
END.
Comments
Post a Comment