TIBA YA KANSA YAPATIKANA.
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/9/9/2015 2:18:57 PM
Tabia Ya Watanzania
Kupuuza tiba mabadala imekuwa sababu kubwa ya kushuka kwa umri wa kuishi
kunakosababishwa na watu wengi kukumbatia mila na desturi za kigeni na kupuuza
utamaduni wetu ikiwa pamoja na ulaji usio na mpangilio.
Hayo
yamebainishwa na DKT.BAHATI MAYALA ambaye ni maarufu kwa kutibi kwa kutumia
tiba mbadala ambayo haiusiani na masuala ya nguvu za kiza, bali kwa kutumia
mimea na miti inayotuzunguka.
DKT.MAYALA
ambaye kwa sasa amewahudumia wagonjwa mbalimbali ambao wanasumbuliwa na Kansa
ya matiti ambao mwandishi wa Habari hizi amebahatika kuwaona na kuongea nao, na
kumeleza jisi hali yao ilivyoimarika mara baada ya kukutana na DKT.MAYALA
ambaye amesomea kazi hiyo.
DKT.MAYALA
ambaye amewahi kufanya kazi katika Hospital ya Mkoa wa Ruvuma kwa takriban
miaka kumi,amesema yeye ameanza kujua miti dawa akiwa na miaka minane na kwa
kupata nafasi kwenda kusomea udaktari kulimpanua akili na kuanza kufanya
utafiti wa miti dawa ambayo inaweza kutibi magonjwa sugu ikiwemo kansa na
UKIMWI.
Mmoja wa
wagonjwa ambaye alikuwa tayari kutoa ushuhuda, BIBI.JOYCE KISAMO ambaye yeye
alikuwa anakabiliwa na kansa ya titi, ambalo lilianza kama uvimbe mdogo ambao
haumi, lakini baada ya kukaa muda mrefu tatizo hilo ndio likaanza kujitokeza.
BIBI.KISAMO
amebainisha kuwa mara akaanza kuona uvimbe katika titi lake unauma na kuanza
kutoa damu na maji machafu, ilifika hatua ambayo hata ndugu zake walikata tama
iwapo kama angeweza kupona.
Lakini
baadaye akatokea DKT. MAYALA na kumpatia dawa ambayo imemsaidia kwa kiasi
kikubwa, ingawa hapo mwanzo alipoaanza kunywa dawa ilimuongezea maumivu, na
alipomuuliza daktari. MAYALA mbona tatizo linazidi, akamueleza aendelea kutumia
dozi na matokeo yake ni nafuu kubwa ambayo ameipata na ile hali ya maumivu
makali ambayo yalimfanya asilale yameisha kwa kiasi kikubwa.
Naye shemeji
wa BIBI.JOYCE KISAMO, BW.FELIX ZACHARIA amesema alimkuta katika hali mbaya,
kabla ya kutumia dawa hiyo, lakini kutokana na kujitokeza kwa DKT.MAYALA
kumeweza kumsaidia na kuweza hata kufanya mazoezi.
BW.ZACHARIA
amewataka Watanzania kutokubali kufa kutokana na kupuuza tiba asilia ambayo
inahusisha matumizi ya miti dawa na vyakula tulivyonavyo, na tusiwapuuze
wataalamu wanajitokeza na wenye uwezo wa kusaidia binadamu wenzao.
END.
Comments
Post a Comment