VIDEO ALALAMIKIA POLICE KIMARA KUMUACHIA MHALIFU WA KUTUMIA SILAHA YA MOTO.



Ben Komba/Pwani-Tanzania/9/27/2015 2:28:03 PM
Vitendo vya Jeshi la Polisi kukiuka maadili ya kazi zao kwa makusudi yamezidi kushika kasi na huku wananchi wakipoteza imani kabisa na Jeshi hilo jambo ambalo linachochea vitendo vya wananchi kujichukulia sheria mkononi.

Hivi karibuni nimekutana na mwananchi ambaye kazi yake ni dereva wa magari ya mizigo, BW.JUMBE RASHID JUMBE ambaye amenielezea mkasa ambao umemkuta baada ya kupaki gari eneo la Kimara Korogwe.

BW.JUMBE amesema siku ya tukio yeye akiwa anaelekea katika gari yake, ndipo wakatokea vijana wawili na BODA BODA na kuanza kumshambulia huku mwenzao akifungua starter ya gari lake, katika tukio hilo alifanikiwa kuwazidi nguvu majambazi yale ambayo yalikuwa na bastola na kuacha pikipiki yao.

Bw.JUMBE baada ya kuona majambazi yale yamekimbia na kumwachia pikipiki ikiwa nay eye anasafiri aliamua kuipeleka kituo cha Polisi Kimara na kukikabidhi pikipiki hiyo sambamba na kuandika maelezo nay eye kuendelea na safari nje ya nchi.

Lakini kinyume chake mara baada ya kuondoka nchini Polisi waliamua kufunga Jalada la kesi hiyo ya wizi wa kutumia nguvu ili hali mtu ambaye amefanya jambo hilo alikuwa anajulikana, halia ambayo inamsononesha sana mwananchi huyo, JUMBE RASHID JUMBE.

BW. JUMBE amewataka Polisi kutimiza wajibu wao bila kuendekeza vitendo vya aina yoyote vya rushwa.

END

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA