WAKULIMA WANALIA NA MIFUGO-VIDEO

Ben Komba/Pwani
Ushirika wa wakulima wa mbogamboga katika Bonde la Mto Ruvu, Kijiji cha Kidogezero Kata ya Lugoba Tarafa ya Msoga, wameiomba serikali kuiifanyia kazi suala zima la ng”ombe kuingia katika mashamba yao,hali inayotishia ustawi wa kiuchumi na kiafya.

Wakazi Bw. Said Msumi na Ally Mwenda kwa niaba ya wenzao waliwaeleza
waandishi wa habari kuwa kero hiyoimekuwa kubwa kiasi cha kuwakatisha
tama kwenye kuendeleza kilimo.


Ameongeza kwamba kutokana na ukweli  huo unapofika wakati wa kilimo
wanalazimika kutumia zaidi ya shilingi laki moja kwa ajili ya kuingiza
trekta badala y ash. 50,000 kwa eka hii hiyo inatokana na ardhi kuwa
ngumu hatua ambayo wamilik wa vyombo hivyo kutoza kiasi hicho.

Kwa upande wake Mwenda amesema wachungaji wanaingiza mifugo katika
mashamba hali inayotishia usalama kwenye maeneo hayo najamii hiyo
inayojihusisha na mifugo.


Akizungumzia changamoto hiyo Mwenyekiti wa kijiji hicho Bw. Ally
Mmanga amekiri kuwepo kwa hali hiyo na kueleza wamewsiliana na uongozi
wa NAFCO uliopo jirani kabisa na kijiji ili kusaidiana kudhibiti hali
hiyo.
END

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA