WATNZANIA WATAKIWA WAMUENZI NYERERE KWA VITENDO.



Ben Komba/Pwani-Tanzania/10/16/2014 11:59:41 AM

Naibu katibu mkuu Bara wa CHADEMA Mbunge wa Ubungo BW.JOHN MNYIKA amewataka Watanzania kuwaangalia kwa makini watu wanaojifanya kumuenzi kwa maneno MWL.JULIUS NYERERE wakati vitendo ni wanavyofanya ni tofauti na wanayoyahubiri majukwaani.

BW.Mnyika ameyasema hayo katika kilele cha maadhimisho ya NYERERE DAY ambayo yameandaliwa Baraza la vijana CHADEMA mkoa wa Pwani ambalo limefanyika wilayani Kisarawe katika mkoa wa Pwani ambapo amesema viongozi wengi wanamtumia baba wa Taifa kwa maslahi binafsi.

BW.MNYIKA ameongeza kuwa Viongozi wengi wa kisiasa hawamuishi NYERERE kama ilivyoelekezwa katika maandiko na hotuba mbalimbali ambazo alizitoa katika kipindi cha uhai wake, aidha amechukua fursa hiyo kukemea utaratibu unaoandaliwa na chama tawala kutumia rejesta za vijiji na mitaa wakati wa zoezi la uchaguzi.`

Naibu katibu huyo Bara alitumia fursa hiyo kuwaeleza vijana wa chama hicho kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania,kuhusiana na mchakato mzima wa katiba ambao ulikuwa katika ilani ya uchaguzi ya CHADEMA na CCM kuamua kuupora na kuuvuruga.

Naye mwenyekiti wa BAVICHA Taifa,BW.PASCHAL KATAMBI akizungumza juu ya katiba, amepinga madaraka makubwa aliyonayo Rais ilihali ambayo kwa kiasi kikubwa ari ya uwajibikaji miongoni mwa watumishi wa serikali, kutokana na uteuzi kufanywa kwa kuangalia undugu,udini na upendeleo.

BW.KATAMBI  amekazia kauli yake kwa kuwaambia washiriki wa kongamano hilo kuwa CHADEMA ina nia ya kweli ya kumkomboa mwananchi wa kawaida kiuchumi,kijamii,kitamaduni, kisiasa na kiuchumi.

END

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA