MFUGAJI MKOROFI
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/31 octoba 2014
Tatizo la
unyanyasaji unaofanywa na wafugaji dhidi ya wakulima limefikia hatua mbaya
baada ya wakulima kushindwa kufanya shughuli zao ambazo zilikuwa zinawapatia
kipato.
RFA ikiongea
na BIBI.MARIAM ALLY Mkazi wa VIGWAZA amesema kuwa anasikitishwa na hatua ya
mfugaji KINDETI kufungulia ng’ombe majira ya usiku na kuanza kura mazao yao,
hali ambayo inawadhoofisha kiuchumi kwani anategemea kazi hiyo kujikimu na hali
ngumu ya maisha.
BIBI. MARIAM
ALLY ameongeza kuwa mara zote wanapoenda kutoa taarifa katika uongozi wa
kijiji, kunakuwa hakuna hatua yoyote
inayochukuliwa kupambana na hali hiyo na hivyo kuwafanya wakulima kuwa
na wakati mgumu kutafakari wataishi vipi baada ya mazao yao kuliwa na mifugo.
Naye BI.HALIMA
TILINDE amesema inapotokea kwenda kuripoti kwenye uongozi wanaambiwa kuwa
wananchotakiwa kufanya ni kukamata mnyama husika na kumfikisha kituo cha
Polisi, jambo ambalo limekuwa gumu kwa upande wao, kutokana na kutokuwa na
uzoefu na shughuli za ufugaji.
Afisa wa
mifugo Kata ya Vigwaza BI.LUCY BALILEMWA amekemea hali inayoendelea hivi sasa
kwa kuwakumbusha wafugaji kutowadharau wakulima kutokana na fedha ambazo wanazo
kulinganisha na wenzao hivyo amewataka kutowanyanyasa wenzao.
BI.BALILEMWA
amebainisha kuwa anaanda mkutano na wafugaji kujua tatizo nini mpaka hali
inakuwa hivyo, na akashauri ni vyema wafugaji wakaweka njia maalum kwa
kupitishia ng’ombe wanapoenda malishoni na kuwaheshimu wenzao.END.
Comments
Post a Comment