SHERIA ZA USHIRIKA ZIMEPITWA NA WAKATI-RC PWANI-VIDEO
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/10/4/2014 1:35:59 AM
Mkuu wa mkoa
wa Pwani BI.MWANTUMU MAHIZA amewataka watendaji katika vyama vya ushirika
kutimiza wajibu wao ipasavyo ili waweze kuvipatia mafanikio yatarajiwayo vyama
hivyo ili kuweza kumkwamua mkulima wa kawaida kutoka katika lindi la umaskini.
BI.MAHIZA
amesema hayo wakati wa kikao cha Bodi ya Korosho kilichofanyika wilayani
Mkuranga, amesema wakati umefika sasa kuzipitia upya sheria za vyama vya
ushirika ili kutoa haki sawa kwa mkulima na hasa ikizingatiwa kuwa sheria
nyingi za ushirika zimelenga kumlinda kiongozi.
Mkuu wa mkoa
wa Pwani BI.MAHIZA ameongeza kuwa imekuwa ngumu kwa chombo chochote kumtia
hatiani kiongozi mbadhirifu yoyote wa ushirika kutokana na kuendelea
kukumbatiwa sheria zilizopitwa na wakati ambazo zinadumaza maendeleo ya
mkulima.
BI.MAHIZA
amefafanua kwa upande wa mkoa wa Pwani wao wamekwenda mbali kiasi cha kumshauri
Waziri mwenye dhamana na kilimo kufikisha Bungeni maoni yao juu ya uwezekano wa
kupitiwa upya sheria za ushirika.
Awali Mwenyekiti
wa Bodi ya Korosho nchini,BW.JUMA YUSUF amesema mwaka jana Mikoa inayolima
korosho ilipatiwa pembejeo kwa ajili ya kuimarisha mavuno ya zao hilo ikiwa na
kuvipatia vyama vya msingi vya ushirika mbegu ya miti ya mikorosho ya kisasa.
END.
Comments
Post a Comment