WLAC WAPONGEZWA KUSAIDIA WANANCHI
Ben
Komba/Pwani-Tanzania
Mkuu wa
wilaya ya Kibaha, BIBI.HALIMA KIHEMBA ameunga mkono harakati zinazofanywa na
mashirika yasiyo ya kiserikali katika utoajai wa usaidizi wa kisheria kwa jamii
ambayo haina uwezo wa kifedha kunufaika na huduma za kisheria zitolewazo.
Mkuu huyo wa
wilaya ameyazungumza hayo wakati akifunga mafunzo kwa wasaidizi wa kisheria
takriban 32 waliopatiwa mafunzo hayo kwa lengo la kwenda kuisaidia jamii
inayowazunguka ambayo inakabiliwa na migogoro lukuki ya kisheria.
Ameongeza kuwa
ni ukweli usiopingika kwa jamii yetu kama jamii nyingine Duniani zinakabiliwa
na migogoro mikubwa ya kisheria, na huku gharama za kutafuta usaidizi wa
kisheria zikiwa zipo juu, na hivyo haki za watu wanyonge kuporwa na wenye
fedha.
Mkuu wa
wilaya KIHEMBA amewapongeza kituo cha usaidizi wa kisheria kwa wanawake na
watoto (WLAC), Kibaha Paralegal Centre na Kibaha Picha ya Ndege Paralegal kwa
kuhakikisha wanajenga uwezo kwa wasaidizi wa kisheria kwa manufaa ya jamii ya wanaKibaha.
Awali
akizunguimza katika ufungaji wa mafunzo hayo ya wasaidizi wa kisheria,
Mkurugenzi wa Mafunzo wa Kituo cha Usaidizi wa kisheria kwa wanawake na watoto,
BI.MAGDALENA MTOLERA amesema Shirika la WLAC limeanzishwa mwaka 2004, na lengo
kubwa ni kuwasaidia wanawake.
END.
Comments
Post a Comment