WAANDAMANA KUDAI HAKI MKOA PWANI-VIDEO
Wananchi wa Kijiji cha Kinzagu kata ya Lugoba Tarafa ya Msoga wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwania wameandamana kudai utekelezaji wa makubaliano kati ya kijiji na mwekezaji.
Wananchi hao waliokuwa wakiimba nyimbo za kudai haki zao kufuatia kuchoshwa na ahadi ya mwekezaji katika madini ya kokoto kijijini hapo kutototekeleza ahadi walizokubaliana wakati walipofika kuomb ardhi kwa ajili ya uchimbaji wa madini ya kokoto kwa matumizi ya ujenzi wa mabasi yaendayo kasi jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa kiji hicho BW. WILLIAM MAKUMU akizungumza kwa niaba ya wakazi amesema kuwa wanaungana na wanakijiji hao kutokana na Kampuni STRABAG kuchukua ardhi kwa makubaliano wa ujenzi wa zahanati lakini baada ya kuchelewa kufanya hivyo moja ya makampuni yanayoenbdesha shughuli za uchimbaji ikajenga hivyo wakaingia makubaliano mengine ya kuwapatia umeme na kununua trekta.
MAKUMU amebainisha kuwa Mkandarasi huyo kampuni ya STRABAG imekuwa ikizunguka katika utekelezaji huo tangu waanze uchimbaji mwaka 2012, hali inayowafanya wananchi kuwa na imani tofauti huenda viongozi wa kijiji na wa kampuni wanawageuka hali ambayo haipo.
BW.MAKUMU ameongeza kuwa mara baada ya kuona suala la zahanati limeshapata ufumbuzi,ndipo mkutano mkuu wa kijiji ulipoamua kumbadilishia mkandarasi huyo kutoka suala la ujenzi wa zahanati hadi kutakiwa kununua trekta na umeme.
Mwakilishi wa kampuni ya STRABAG, BW.JOHN URRASA amewahakikishia wananchi wa Kinzagu kuwa watulivu nay eye kama mwakilishi wa kampuni hiyo atafikisha ujumbe huo kwa viongozi wa juu wa STRABAG.
End.
Comments
Post a Comment