KIBAFA WAPATA UDHAMINI



Ben Komba/Pwani-Tanzania

Chama cha soka wilayani Kibaha-KIBAFA- kimempata mdhamini wa kuendesha ligi ya daraja la nne wilayani hapa.

Mwakilishi wa vilabu wilaya ya Kibaha, MRISHO KHALFAN amebainisha kuwa wamempata mdhamini ambaye atachukua jukumu lote la uendeshaji wa ligi ya soka daraja la nne wilayani Kibaha.

KHALFAN amesema kuwa Mdhamini huyo anayekwenda kwa jina la DOKTA MICHAEL MTALI ambaye kwa upande wake amekuwa akijishughulisha bna masuala mbalimbali ya michezo ikiwa pamoja na kumiliki timu ya soka ya wanawake.

Aidha mwakilishi wa vilabu wilayani Kibaha, MRISHO KHALFAN ameongeza kuwa mpaka sasa timu 12 zimeshachukua fomu kwa ajili ya kushiriki mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza Oktoba 30.

END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA