Ben Komba/Pwani-Tanzania/05-May-12/06:53:40 PM
Mtu anayesadikiwa ni moja kati ya majambazi waliovamia nyumbani kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha wananchi wilayani Kibaha, BW. UWESU FADHILI amekutwa amekufa baada ya kujeruhiwa tumboni na kitu chenye ncha kali.
Mwandishi wa habari hizi ameshuhudia mwili huo ukiwa umeharibika kwa kiasi cha asilimia 70, huku wadudu wakiushambulia, baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walimtambua marehemu kama mmoja wa vijana wanaokaa katika nyumba ya Mwenyekiti wa kitongoji cha DENGWA ambaye kwa sasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoa wa Pwani BW. SHAABAN MISALE aka KANGEME.
Na kushikiliwa kwake kunahusiana na tukio la kwanza ambapo askari waliokuwa doria walifanikiwa kukabiliana na majambazi hayo na kufanikiwa kumuuwa Jambazi SALUM HAMIS aka MAPOZI, ambaye baada ya kufuatiliwa taarifa zake ikagundulika anakaa nyumbani kwa mwenyekiti huyo anayeshikiliwa.
Mwenyekiti wa kijiji cha Vikuge, BW. VITUS MCHAMI amebainisha taarifa kuhusiana na uwezekano wa kutokea tukio hilo zilijulikana mapema na kwa upande wake uongozi wa kijiji ulijipanga kukabiliana na jaribio hilo ikiwa pamoja na kutoa taarifa kituo cha Polisi ambao nao kwa upande wao waliweka doria ambapo katika siku ya kwanza ya ulinzi kuzunguka maeneo ya makazi ya marehemu majahili hao hawakutokea.
Na ndipo Jeshi la Polisi likawataka wale viongozi waliojitolea kulinda makazi hayo kuendelea na utaratibu wao wa kawaida na wao watahakikisha wanamlinda Mzee asipate madhara kwa gharama yoyote, na hivyo wao kuamua kusitisha zoezi la kulinda.
Mwenyekiti huyo wa kijiji BW. MCHAMI amebainisha kuwa na ndipo siku ya Mei mosi mwaka huu majira ya alfajiri majambazi hayo yakavamia nyumbani kwa mzee huyo ambaye alijaribu kupambana nao, kwa kutumia mkuki ambapo inasemekana alijeruhi baadhi ya majambazi na mmoja aliyeingia mwanzo ndio aliyekutana na mkuki uso kwa uso, lakini majambazi wenzake wakamburuta na kwenda kumtelekeza.
Mwenyekiti wa kiji cha Vikuge amechukua fursa hiyo kukanusha kuwa mauaji hayo ni ya kisiasa, kwani kumekuwepo na matukio mengi ya aina hiyo kunakosababishwa na kutokuwepo kwa kituo cha Polisi maeneo ya jirani.
END.
Comments
Post a Comment