HALMASHAURI YA WILAYA YA KIBAHA NA RIPOTI YA UKAGUZI


Ben Komba/Pwani-Tanzania/2012-05-24/17:33:26 Halmashauri ya wilaya ya Kibaha ya Kibaha kupitia kikao maalum cha Baraza la madiwani, imesoma taarifa ya ukaguzi wa mahesabu ya kipindi cha mwaka wa fedha 2010/2011 ambayo imebainisha maendeleo ya miradi mbalimbali yenye lengo la kusaidia jamii katika huduma muhimu kama za maji, ujenzi wa miundombinu na utawala. Akisoma taarifa hiyo Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha anayeondoka, BI. AZIMINA MBILINYI, ambaye anakwenda kuwa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero amesema katika kipindi chake kuna kiasi cha shilingi milioni 32,890,673/=, ambapo zimenuwiwa kuelekezwa kwenye mradi wa ujenzi wa stendi ya mabasi Mlandizi, Na tayari maelekezo yameshatolewa kutengenezwa kwa mpango kazi ambao ambao utatoa mchanganuo wa matumizi ya fedha ambazo zinakadiriwa kufikia shilingi Milioni 30 zitatumbukizwa katika utekelezaji wa mradi huo,m ikiwa na pamoja na shilingi milkiuoni 2,890,00/= kwa ajili ya usimamizi wa mradi huo, na mapendekezo ya kamati ya fedha, uongozi na Mipango ya halmashauri ya wilaya ya Kibaha ilipendekeza kuwepo kwa ufuatiliaji wa karibu wa utekelezaji wa mradi huo. Mwenyekiti wa Baraza la madiwani halmashauri ya wilaya Kibaha, BW. MANSOOR KISABENGO amempongeza Mkurugenzi huyo kwa kuanzisha miradi mbalimbali imkiwa pamoja na ujenzi wa stendi ya Mlandizi, Mradi wa upimaji wa viwanja ambao unategemewa kuipatia halmashauri fedha kutokana na gharama zitakazotozwa kwa watu watakahoitaji viwanja hivyo. BW. KISABENGO ameongeza katika kipindi cha miaka miwili chini ya Mkurugenzi huyo halmashauri ya wilaya ya Kibaha imefanikiwa kusambaza matrekta kwa ajili ya kuunga mkono hatua ya serikali ya kutoa kipaumbele kwa kilimo kupitia sera yake ya kilimo kwanza katika kuhakikisha maendeleo endelevu yanapatikana wilayani Kibaha. END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA