KIONGOZI WA CCM AKANUSHAKUJIHUSISHA NA USHOGA.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/04/15/13/19:32:10 Katibu wa uchumi, malezi na mazingira wa chama cha mapinduzi Kata ya Mailimoja BW. LAZARO KULIGWA amekanusha kuhusika kwake na ufanyaji wa mapenzi ya jinsia moja kama inavyosambazwa na mahasimu wake wa kisiasa ndani ya chama hicho kwa lengfo la kumharibia mafanikio ambayo ameyapata katika medani ya siasa. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisi ya CCM wilaya ya KIBAHA, BW. KULIGWA amesema kuwa yeye binafsi kwa kipindi kirefu sasa amekuwa akisikia watu wakimsema chinichini na alikuwa anangoja mwenye kujitokeza amuulize kuhusiana na hilo lakini hakutokea mpaka alipokutana na mwandishi wa hizi. BW.KULIGWA amebainisha kuwa kwa mara ya kwanza ilikuwa wakati wa kampeni ya uchaguzi mkuu uliopita ambapo mmojka wa wagombea alikusanya vijana na kujenga maneno hayo kwa lengo la kumharibia kisiasa ingawa mpaka sasa anasubiri mtuwa kujitokeza kuthibitisha madai hayo ambayo yana lengo la kumchafua. Akizungumzia kuibuka kwa maneno hayo ya kumhusisha na mapenzi ya jinsia moja,inatokana na yeye kamaKatibu wa uchumi, malezi namazingira wa kata ya Maili kluamua kuzitambua mali mbalimbali za Jumuiya ya wazazi kwa lengo la kuzihakiki na kuziendelezakwa faida ya chama kitu kinachuwauzi baadhi ya watu. Hata BW.KULIGWA ameelezea kutotetereshwa na maneno hayo kwani ameshabaini mbinu ya wahasimu wake wa kisiasaa ya kutengeneza maneno ambayo hayajengi mshikamano katika chama na matokeo yake yanakibomoa chama, Na amelaumu uongozi wa CCM mjini Kibaha kwa kutotafuta ufumbuzi wa busara kuhusiana na tuhuma hizo zenye lengo la kumuaibisha mtu binafsi. END

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA